|
بسم الله الرحمن الرحيم
الدعوة الإسلامية بالسواحلية
أولا: روابط
الدعوة الإسلامية بالسواحلية
http://www.geocities.com/Athens/Parthenon/2355/
http://www.religionofislam.com/swahili/index.htm
ثانيا: الرسائل الدعوية بالسواحلية
تعريف
موجز بالإسلام
باللغة : السواحلية
Introduction to Islam in Swahili Language
MAELEZO KWA UFUPI KUHUSU UISLAMU
Kila sifa njema ni zake Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe
vyote, sala na amani ziwe juu ya Imamu wa Mitume, Nabii
wetu Muhammad, na jamaa zake, na Masahaba wake wote.
Ama baada:_
UISLAMU:_ ni kushuhudia kuwa hapana Mola apasae
kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu mmoja, na Muhammad
(rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) ni
mjumbe wa Mwenyezi Mungu, (kushuhudia) kwa moyo, na kwa
ulimi, na kwa viungo.
Na (huo Uislamu) unajumuisha kuamini nguzo sita za Imani
kwa kutekeleza nguzo tano za Uislamu, na nguzo mbili za
Ihsani.
Na (huo Uislamu) ni risala ya mwisho miongoni mwa risala
za Mwenyezi Mungu, ambayo ameiteremsha Mwenyewe Allah
kwa mwisho wa manabii wake na mitume wake, Mtume
Muhammad bin Abdillah (rehema na amani za Mwenyezi Mungu
ziwe juu yake).
Na (huo Uislamu) ndiyo dini ya haki ambayo Mwenyezi
Mungu hatakubali dini nyingine isiyokuwa uislamu, na
hakika ameifanya Mwenyezi Mungu dini ya uislamu kuwa
nyepesi na rahisi, hakuna ugumu au uzito ndani yake,
wala tabu, hakuwalazimisha (Allah) wenye kuingia ndani
ya dini hiyo mambo wasiyo yaweza, na wala
hakuwakalifisha kwa yale wasiyoweza.
Na ni dini ambayo msingi wake ni TAUHID (kumpwekesha
Mwenyezi Mungu katika ibada), na alama yake ni ukweli,
na imezungukwa na uadilifu, na ndiyo usimamizi wa haki,
na roho yake (dini hii) ni huruma, na ni dini tukufu
ambayo huwaongoza waja (watu) kwenye kila jambo lenye
manufaa katika dini yao na dunia yao, na
huwatahadharisha kutokana na kila lenye madhara katika
dini yao na maisha yao,
Na ni dini ambayo Mwenyezi Mungu amerekebisha kwayo
itikadi na tabia, na akarekebisha kwayo maisha ya
duniani na Akhera, na akaziunganisha kwayo nyoyo zilizo
tafautiana, na matamanio mbali mbali, akazisafisha
kutokana na sifa za upotofu, na akazielekeza kwenye
haki, na akaziongoza kwenye njia iliyo nyoka.
Na ni dini iliyo sawa iliyo kamilika isiyokuwa na kasoro
katika habari zake zote, na hukumu zake zote,
haikuelezea ila ukweli na haki, na wala haikuhukumu ila
kwa kheri na uadilifu, miongoni mwa itikadi sahihi, na
vitendo vilivyo sawa, na tabia bora, na desturi za hali
ya juu.
Na ujumbe wa Uislamu unalengo la kutimiza mambo
yafuatayo:
~ Kuwajulisha watu mola wao na muumba wao kwa majina
yake mazuri ambayo hakuna mwenye majina hayo isipokuwa
yeye tu, na sifa zake za hali ya juu ambazo hakuna
mwenye kufanana nae katika sifa hizo, na vitendo vyake
vya hekima ambavyo hana mshirika kwenye vitendo hivyo,
na kustahiki kwake ambako hana mshirika ndani yake.
~ Kuwalingania waja (watu) ili wamuabudu Mwenyezi Mungu
pekeyake hana mshirika, kwa kufuata mambo aliyo wawekea
sheria katika kitabu chake (Qurani) na Sunna za mtume
wake (Muhammad rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe
juu yake) miongoni mwa maamrisho, na makatazo ambayo
ndani yake mna kutengenea kwao katika dini yao, na
akhera yao.
~ Kuwakumbusha hali yao na marejeo yao baada ya kufa na
mambo watakayo kutana nayo ndani ya makaburi yao, na
wakati wa kufufuliwa kwao , na kuhesabiwa kwao, na
mwisho wao ima peponi au motoni. Mwenyezi Mungu
atawalipa kulingana na matendo yao, aliye tenda wema
atalipwa wema, na aliye tenda uovu atalipwa uovu.
Na tunaweza kufupisha misingi muhimu ya Uislamu kwenye
nukta zifuatazo:-
NUKTA YA KWANZA: NGUZO ZA IMANI
NGUZO YA KWANZA:- NI KUMUAMINI MWENYEZI MUNGU MMOJA.
Nayo inajumuisha mambo yafuatayo:-
A-Kuamini kuumba kwake Mwenyezi Mungu mtukufu, yaani
kuamini kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mola Muumba mwenye
kumiliki kila kitu, mwenye kuendesha mambo yote ya
viumbe vyake, mwenye uwezo wa utendaji kazi kwao.
B-Kuamini kuwa ibada ni kuabudiwa Mwenyezi Mungu
mtukufu, yaani kuamini kuwa yeye Mwenyezi Mungu ndiye
Muabudiwa wa haki, na kila kiabudiwacho asiyekua
Mwenyezi Mungu ni batili.
C-Kuyaamini majina yake, na sifa zake Mwenyezi Mungu,
yaani kuamini kuwa yeye Mwenyezi Mungu ana majina
mazuri, na sifa zilizokamilika za haliya juu, kwa namna
yalivyokuja katika kitabu chake, na Sunna za Mtume wake
(rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)
NGUZO YA PILI:- KUAMINI MALAIKA
MALAIKA: ni viumbe na waja walio tukuzwa, aliwaumba
Mwenyezi Mungu mtukufu, wana muabudu, na wanamtii, na
akawapa kazi tofauti tofauti.
Miongoni mwa hao ni: Jibril ambae alipewa kazi ya
kuteremsha Wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa amtakae
katika manabii wake, na mitume wake. na miongoni mwa hao
ni: Mikael aliyepewa kazi ya mvua, na mimea. na miongoni
mwa hao ni: Israfil aliyepewa kazi ya kupuliza Baragumu
wakati wa kutolewa viumbe vyote roho zao (mwisho wa
dunia) na wakati wa kufufuliwa. na miongoni mwa hao
Malaika ni Malaika wa mauti aliyepewa kazi ya kutowa
roho wakati wa kufa.
NGUZO YA TATU:-KUAMINI VITABU
Mwenyezi Mungu mwenye nguvu na aliyetukuka aliteremsha
vitabu kwa Mitume wake, ndani ya hivyo vitabu mna
uongofu na kheri na utengenefu. Na tunavyovijuwa
miongoni mwa vitabu hivyo ni:-
A-TAURATI:
Aliiteremsha Mwenyezi Mungu kwa Mtume Musa (rehema na
amani ziwe juu yake). Na ni kitabu kitukufu cha Wana wa
Israili.
B- INJILI:
Ambayo aliiteremsha Mwenyezi Mungu (Aliyetukuka) kwa
Mtume Issa (sala na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu
yake).
C- ZABURI:
Ambayo Mwenyezi Mungu (Aliyetukuka) alimpa Mtume Daudi
(rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake).
D- NYARAKA:
Alizopewa Nabii Ibrahimu, na Mtume Musa, (rehema na
amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao).
E- QURANI TUKUFU:-
Ambayo Mwenyezi Mungu (Aliyetukuka) aliiteremsha kwa
Nabii wake Muhammad (rehema na amani za Mwenyezi Mungu
ziwe juu yake), mwisho wa Manabii wote, Mwenyezi Mungu
akafuta kwayo (hiyo Qurani) Vitabu vyote vilivyo
tangulia, na akachukuwa jukumu la kuihifadhi (hiyo
Qurani) kwasabu itabaki kuwa hoja juu ya viumbe vyote
hadi siku ya kiyama.
NGUZO YA NNE:-KUWAAMINI MITUME.
Mwenyezi Mungu aliyetukuka aliwatuma Mitume kwa viumbe
vyake, na wa kwanza wao (hao mitume) ni Nuhu, na wa
mwisho wao ni Muhammad (rehema na amani za Mwenyezi
Mungu ziwe juu yao. Na Mitume wote wakiwemo Issa mwana
wa Mariyamu, na Uzeir (rehema na amani za Mwenyezi Mungu
ziwe juu yao) na Salama, ni wanadamu walioumbwa, hawana
sifa zozote za uungu. Wao ni waja miongoni mwa waja wa
Mwenyezi Mungu, aliwatukuza (mwenyewe) Mwenyezi Mungu
aliyetukuka kwa (kuwapa) ujumbe (kwa viumbe wake) na
amekamilisha Mwenyezi Mungu wajumbe wote kwa ujumbe
aliokuja nao Mtume Muhammad (rehema na amani za Mwenyezi
Mungu ziwe juu yake), na akamtuma kwa watu wote. Hakuna
(Mtume wala) Nabii mwingine baada yake (Mtume Muhammad
rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake).
NGUZO YA TANO:KUAMINI SIKU YA MWISHO.
Nayo ni siku ya Qiyama, ambayo hakuna siku nyingine
baada yake, wakati Mwenyezi Mungu atawafufuwa watu wawe
hai ili wabaki ima katika nyumba ya neema (peponi), na
ima katika nyumba ya adhabu iumizayo (motoni). Na
kuiamini siku ya mwisho ni kuamini kila jambo
litakalokuwa baada ya kufa.
Miongoni mwa mitihani ya kaburini na starehe zake na
adhabu zake, na yatakayotokea baada ya hapo kama
kufufuliwa, na kutawanyika, na hesabu, kisha iwe pepo au
moto.
NGUZO YA SITA:KUAMINI KADARI
Kadari ni kuamini kwamba Mwenyezi Mungu alikadiria kila
kitu, na akaumba viumbe kulingana na elimu yake
iliyotangulia, na namna alivyotaka kuwa kutokana na
hekima yake. Mambo yote Mwenyezi Mungu (Aliyetukuka)
ayajuwa kwa elimu yake ya hapo awali, na yameandikwa
kwenye Lauhil Mahfudh (Ubao ulio hifadhiwa), na Mwenyezi
Mungu aliyataka na akayaumba yote, hakuna jambo lolote
lenye kutokea ila kwa kutaka kwake, na kutengeneza
kwake, na kuumba kwake.
NUKTA YA PILI: NGUZO ZA UISLAMU
Uislamu umejengwa juu ya nguzo tano. Na mtu hawi
Muislamu wa sawa sawa mpaka aziamini, na azitekeleze,
nazo ni:-
NGUZO YA KWANZA: SHAHADA MBILI.
Ni kushuhudia kwamba hakuna Mola apasae kuabudiwa kwa
haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na Muhammad ni mtume wa
Mwenyezi Mungu, na huku kushuhudia ndiwo Ufunguo wa
Uislamu, na Msingi wake ambao hujengwa juu yake.
Na maana ya LA ILAHA ILLA LAHU yaani hakuna apasae
kuabudiwa kwa haki isipokua Mwenyezi Mungu peke yake,
yeye ndie Muabudiwa wa haki,na kila chenye kuabudiwa
asiye kuwa Mwenyezi Mungu ni Batili. Na ILAHU maana yake
ni:-mwenye kuabudiwa.
Na maana ya kushuhudia kwamba Muhammad ni Mtume wa
Mwenyezi Mungu:- Ni kukubali yale aliyoeleza, na kumtii
katika yale aliyoamrisha, na kujiepusha na yale
aliyoyakataza na akayakemea na asiabudiwe Mwenyezi Mungu
ila kwa namna alivyo weka sheria.
NGUZO YA PILI: SALA
Nazo ni Sala tano katika nyakati tano usiku na mchana,
Aliziwekea sheria Mwenyezi Mungu ili ziwe ni utekelezaji
wa haki yake Mwenyezi Mungu ambayo inawalazimu waja
wake, na ziwe ni kushukuru neema zake Mwenyezi Mungu, na
mfungamano baina ya Muislamu na Mola wake anamnong’oneza
ndani yake na anamuomba, na ili ziwe ni zenye kumzuia
Muislamu kutokana na mambo machafu na maovu, na
akazifanya kuwa ni dini bora, na kutengenea kwa imani,
na Thawabu za papo hapo na za baadae. Mja hupata kwa
hizo Sala raha ya nafsi, na ya mwili, ambayo humfanya
kufaulu duniani na akhera.
NGUZO YA TATU: ZAKA
Nayo ni sadaka ambayo huitowa yule inaye mlazimu, kila
mwaka kwa wanaostahiki kupewa, miongoni mwa Mafukara na
wengineo miongoni mwa wale wanao faa kupewa Zaka, na
hiyo Zaka si lazima kwa fukara ambae hana kiwango cha
Zaka, lakini nilazima kwa matajiri, ili kutimiza dini
yao, na Uislamu wao, na kuziendeleza hali zao, na tabia
zao, na kuwaondoshea maafa wao na mali yao, na
kuwatakaza kutokana na makosa, na kuwahurumia wenye
kuhitaji, na mafukara, na kusimamia maslahi yao yote, na
hiyo Zaka pamoja na hilo, ni fungu dogo sana
ukilinganisha na kile alicho wapa Mwenyezi Mungu
miongoni mwa mali na riziki.
NGUZO YA NNE:SAUMU
Nayo ni kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani, mwezi wa
tisa miongoni mwa miezi inayokwenda kwa hesabu za
kimwezi kwa kalenda ya kiislamu. Katika mwezi huo wa
Ramadhani Waislamu huwacha kila kitu chenye kutamanisha,
au kusababisha kufunguwa, kama vile kuwaingilia wake zao
mchana wa ramadhani, kunywa, kula, na kadhalika, kutoka
kuchomoza alfajiri mpaka kuzama kwa jua, na huwalipa
Mwenyezi Mungu kutokana na hilo miongoni mwa fadhila
zake, na hisani yake, kukamilika dini yao, na imani yao,
na kuwasamehe maovu yao, na kuwapandisha daraja zao, na
mengineyo miongoni mwa yale aliyo yaweka kwenye Saumu
miongoni mwa kheri kubwa katika dunia na akhera.
NGUZO YA TANO:-HIJA
Nayo ni kuitembelea Nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu
(Al-Kaaba) kwa ajili ya kutekeleza ibada makhsusi katika
wakati makhsusi kama inavyo eleweka katika sheria ya
kiislamu, ameifanya Mwenyezi Mungu (Hija) kuwa lazima
kwa anae weza, katika umri mara moja, na katika hiyo
Hija hukusanyika Waisilamu katika eneo bora (Makka)
kutoka kila sehemu, wanamuabudu Mola mmoja, wanavaa nguo
aina moja, hakuna tofauti baina ya kiongozi na raiya, na
tajiri na fukara, na mweupe na mweusi, wanatekeleza
ibada maalum.
Miongoni mwa hizo ibada tukufu ni:-
A-Kusimama kwenye uwanja wa Arafat.
B-Kuizunguka Al-Kaaba Tukufu (Kibla cha Waislamu).
C-Kutembea baina ya Safa na Marwa.
Na ndani ya hiyo Hija mna manufaa mengi ya kidini, na ya
kidunia ambayo hayahesabiki.
NUKTA YA TATU:IHSAN
Ni kumuabudu Mwenyezi Mungu aliyetukuka kwa imani na
kujisalimisha (kwake) kama kwamba unamuona na ukiwa
haumuoni basi yeye anakuona, yaani uhisi hivyo, na
uifanye kwa namna Sunna ya mtume wake Muhammad (rehema
na amani za MwenyeziMungu ziwe juu yake) inavyoeleza na
bila ya kuikhalifu.
Na yote yaliyotangulia yanakusanya maana ya Dini ya
Kiislamu. Na ina eleweka ya kwamba Uislamu umekwisha
panga maisha ya watu wake wakiwa mmoja mmoja, na wakiwa
makundi makundi, kwa mambo ambayo yanawapa ufanisi
katika dunia na akhera. Ukawahalalishia kuowa na
ukawahimiza, na ukawaharamishia zinaa na liwati na mambo
yote mabaya. Na ukawalazimisha kuunga jamaa na
kuwasikitikia mafukara na maskini, na kuwatumikia, kama
ulivyolazimisha na kuhimiza katika kila tabia iliyo
njema, na ukaharamisha na kutahadharisha kutokana na
kila tabia mbaya, na ukawahalalishia pato zuri (halali)
kwa kupitia biashara na ukodishaji, na mfano wa hayo. Na
ukaharamisha riba, na kila biashara iliyo haramishwa, na
kila jambo lenye ulaghai na udanganyifu.
Kama ulivyotambuwa Uislamu tafauti ya watu kutengenea
(kunyoka) katika njia yake, na kuchunga haki za wengine.
Ukaweka sheriya za adhabu zenye kukemea baadhi ya
uvukaji mipaka inayofungamana na haki zake (Mwenyezi
Mungu aliyetakasika), kama kutoka kwenye Uislamu na
zinaa, na kunywa pombe, na makosa mengine kama hayo.
Kama ulivyoweka sheria za adhabu zenye kukemea uvamizi
wa aina yoyote wa haki za watu katika nafsi zao na mali
yao na heshima zao kama: kuuwa, au kuiba, au kumsingizia
mtu (kuwa amezini bila ya kuwa na mashahidi) au uvamizi
kwa kupiga na kuudhi na kuchukuwa mali za watu pasina
haki. Na ni adhabu zenye kulingana na kosa bila ya
kuongeza wala kupunguza,
Kama ulivyopanga na ukaweka mipaka na uhusiano baina ya
raiya na viongzi. Na ukawalazimisha raiya kuwatii
(viongozi), katika mambo yasiyopelekea kumuasi Mwenyezi
Mungu. Na ukaharamisha kutoka katika amri zao hali
itakayo pelekea ufisadi kwa watu wote kwa jumla na kwa
watu binafsi.
Na mwisho tunaweza kusema kuwa Uislamu umefungamana na
kujenga na kuweka uhusiano sahihi, na matendo sahihi
baina ya mja na Mola wake, na baina ya mwanadamu na
jamii yake katika mambo yake yote, hakuna kheri yoyote
miongoni mwa tabia na utendajikazi isipokuwa Uislamu
umekwisha uongoza Umma wake, na ukawahimiza kwayo, na
hakuna shari yoyote katika tabia na utendaji kazi ila
Uislamu umekwisha utahadharisha Umma wake, na
ukawakataza, jambo ambalo lina bainisha ukamilifu wa
dini hii, na uzuri wake katika pande zote.
Na kila sifa njema ni za Mwenyezi Mungu
Mola wa viumbe vyote.
المصدر: موقع الشمسي
إخوة الاسلام
وأحبائنا فى الله شاركونا بابحاثكم ودراساتكم من خلال
مراسلتنا
اضغط هنا
.
بسم الله الرحمن
الرحيم "اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ (1) خَلَقَ
الْإِنْسَانَ مِنْ عَلَقٍ (2) اقْرَأْ وَرَبُّكَ
الْأَكْرَمُ (3) الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ (4) عَلَّمَ
الْإِنْسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ (5)" سورة العلق.
على إسم الله والشورى ، جعلنا الدين دستورا ، وسرنا في طريق الحق ، كان كتابنا النورا |